Mama mwenye nyumba amchoma kisu hausigeli kwa tuhuma za "kutembea" na mumewe
Mama mwenye nyumba amchoma kisu mfanyakazi wake wa ndani (hausigeli) baada ya kumtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mumewe (baba mwenye nyumba.)
Advertisement
Tukio hilo limetokea kijijini Leganda katika wilaya ya Arumeru, Arusha. Inasemekana mama huyo alimhisi mfanyakazi wao, Agel Lema (22), kuwa “anatembea” na mumewe, jambo ambalo lilimfanya amtendee unyama huo.
Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Meru, Dk. Azizi Msuya, alithibitisha kumpokea msichana huyo akiwa na hali mbaya kutokana na jeraha la tumboni. “Lakini binti huyu tulipomhoji, kwanza alikataa na kudai kujichoma mwenyewe, ila baadaye ilibainika alichomwa na mama mwenye nyumba kwa hisia za kufanya mapenzi na mumewe na kumeonya asimtaje kuwa ndiye amemchoma kisu,” alisema Dk Msuya.
Dk. Msuya alisema kutokana na ukubwa wa jeraha, alilazimika kumfanyia upasuaji ili kufanya uchunguzi zaidi. “Tulipomfanyia upasuaji tuligundua hajaathirika utumbo na ulikuwa salama, tukamshona,” alisema Daktari huyo. “Lakini cha ajabu kidonda kikiwa kibichi, msichana huyo alitoroshwa usiku Oktoba 14, kitendo kilichotushangaza,” aliongeza.
Alisema baada ya kugundua hilo, walitoa taarifa Polisi, ili kuokoa maisha ya msichana huyo.
Baada ya kupigiwa simu kuhusu suala hilo, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema hana taarifa.
“Mimi sina taarifa, lakini tukio hilo linaweza kuwapo … kwa kuwa niko mbali huku Moshi kwenye maziko ya Kamanda Barlow (Liberatus), bado sijapata muda wa kufuatilia taarifa za huko na kupata habari zaidi, lakini pia huku mawasiliano yanasumbua sana,” alisema. Kamanda Sabas aliahidi kulifuatilia suala hilo mara atakapopata nafasi na kutoa taarifa.
Chanzo cha habari na picha: Ziro99

Kamanda Liberatus Sabas

![kimara[1]](http://laivu.com/habari/files/2013/02/kimara1-120x120.jpg)